3 Septemba 2025 - 23:42
Source: Parstoday
Russia: Udikteta wa kiliberali wa Magharibi unaeneza chuki duniani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Russia amesema kuwa, ‘udikteta huria wa Magharibi’ unaeneza chuki ulimwenguni kote kwa kasi ya kutisha.

"Moscow imejitolea kukabiliana na chuki dhidi ya wageni inayoshajiishwa na kuenezwa na nchi za Magharibi," Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova ameliambia shirika la habari la Russia Today.

Ameyasema hayo wakati Rais Vladimir Putin akihitimisha ziara yake ya siku nne nchini China kwa kuhudhuria gwaride la kijeshi mjini Beijing leo Jumatano, kuadhimisha miaka 80 ya kushindwa kwa Japan katika Vita vya Pili vya Dunia.

Zakharova amesema kwamba, jitihada za baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari za kudharau au “kupotosha” ushindi wa Urusi na China katika Vita vya Pili vya Dunia zinaonyesha kwamba “ufashisti, Unazi, ubaguzi wa rangi, na chuki dhidi ya wageni haujatokomezwa kabisa duniani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Russia amebainisha kuwa, Moscow inataka kuwepo ushindani wa kiadilifu na kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Amewakosoa vikali viongozi wa Magharibi kwa kuwatazama washindani wao kwa jicho la uadui.

Zakharova ameeleza bayana kuwa, Russia itaendelea kupinga majaribio yoyote ya kupotosha na propaganda kuhusu urithi na historia ya Vita vya Pili vya Dunia.

Your Comment

You are replying to: .
captcha